Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa mikopo ya asilimia kumi (10%) ya kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa vikundi vipatavyo 111 vikijumuisha vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu.
Kata ya Chang'ombe imempongeza Diwani wao Mhe. Bakari Fundikira kwa jinsi anavyoshughulikia kero za elimu na afya katika Kata hiyo.
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti imetembelea Soko la Wazi la Wamachinga Jijini Dodoma na kupongeza utekelezaji wa ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipoagiza wamachinga watafutiwe maeneo na wapangwe kwa utaratibu mzuri utakaowawezesha kufanya shughuli zao vyema.
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.