Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 katika Mtaa wa Ndachi na kuwawezesha wananchi kupata hati za kumiliki maeneo yao kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi Mafuru ametatua mgogoro huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa michezo katika Mtaa wa Ndachi uliopo Kata ya Mnadani jijini hapa. Mafuru amefafanua kuwa wananchi hao wamekosa maendeleo kwa muda mrefu kutokana na kuwa na migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.
SERIKALI imesema inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Watanzania wabunifu katika eneo la elimu, uvuvi, viwanda, kilimo na maeneo mengine.
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeendeleza jitihada katika kukuza sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu na upanuzi wa shule Jijini hapa ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) pamoja na taasisi nyingine za kifedha nchini.
TEA na Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimrfanya hafla ya makabidhiano rasmi ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule za msingi Kisasa, Kizota, Medeli na Mlimwa C jana tarehe Mei 6, 2021 ambapo mradi huo unafanyika chini ya mshauri elekezi Chuo cha Sayansi Mbeya (MUST Consultancy Bereau - MCB) wenye gharama ya shilingi Bilioni 1.9 na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi minne kutoka sasa.
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.