• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wanafunzi UDOM waaswa kuishi kwa kuzingatia maadili

Imewekwa tarehe: November 26th, 2022

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuishi kwa kuzingatia maadili ya kitanzania ili kutimiza malengo yao kitaaluma na kujenga taswira nzuri ya chuo katika jamii.

Ndejembi ametoa nasaha hizo jijini Dodoma, wakati akifunga Kongamano la Kukuza Maadili na Elimu ya Mapambano Dhidi ya Rushwa kwa wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho lililofanyika katika ukumbi wa Chimwaga.

Ndejembi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejipambanua kusimamia utawala bora, kuzingatia maadili na ndio maana inapinga vitendo vya rushwa hivyo, wanafunzi wa UDOM wanapaswa kuzingatia maadili mema kwa lengo la kujenga taswira nzuri ya chuo, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kujenga taifa lenye uadilifu.

"Mnapaswa kuishi kwa kuzingatia maadili ya Kiafrika na Kitanzania kwa sababu tabia zote mbaya mtakazozifanya, jamii haitowaelewa na itakishushia hadhi Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho Serikali inakitegemea katika kuzalisha rasilimaliwatu yenye tija katika maendeleo ya taifa," Ndejembi amesisitiza.

Ndejembi amefafanua kuwa, hata chuo kikiendelea kuwa na matokeo mazuri ya wanafunzi kwa kiwango kikubwa lakini wanafunzi na watumishi wa chuo wasipoishi kwa kuzingatia maadili itakuwa ni sawa na kazi bure kwani hakitakuwa na hadhi mbele ya jamii.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuwa mabalozi wazuri wa kupinga vitendo vya rushwa katika kipindi chote wanapokuwa chuoni na hata baada ya kuhitimu.

Ndejembi amewataka washiriki wa kongamano hilo, kuhakikisha wanafanya mjadala utakaolenga kulinda na kukuza maadili kwa maslahi mapana na mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Matangazo

  • Salamu za heri ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan January 27, 2023
  • Taarifa kwa Umma January 17, 2023
  • Salamu za heri ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar January 12, 2023
  • Heri ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar January 12, 2023
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Dkt. Mabula ataka mafunzo ya maadili kwa madalali

    January 30, 2023
  • Waziri Mkuu awasisitiza wabunge washiriki michezo

    January 29, 2023
  • Viongozi toeni motisha kwa walimu

    January 27, 2023
  • Wananchi waaswa kutumia fursa zinazotolewa na benki za ndani ya nchi

    January 27, 2023
  • Angalia zote

Video

Bwawa la Mtera kuhudumia Dodoma
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    3 CDA Street

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.