• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Tanzania yapata Bil. 240 kuboresha elimu nchini

Imewekwa tarehe: January 16th, 2020

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea msaada wa Dola zaMarekani milioni 90 sawa na shilingi bilioni 240.95 kutoka Mfuko wa Ushirikianowa Elimu Duniani (GPE), kwa ajili ya kugharamia miradi miwili ya Sekta yaElimu.

Mikataba ya msaada huo imesainiwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha naMipango jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James kwaupande wa Serikali na Balozi wa Sweden nchini, Bw. Anders Sjoberg, ambaye nchiyake ni Wakala wa Msaada huo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la nchihiyo (SIDA).

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya msaada huo, Katibu Mkuuwa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James alisema msaada huo ni kwa ajiliya kugharamia miradi ya Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2016/17 –2021/22  na nyongeza ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EP4R).

“Kati ya fedha hizo za msaada, dola za Marekani milioni 38.89 (Sh. bil.88.55) zitatumika kughagharamia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP)2016/17 – 2021/22 na dola za Marekani milioni 51.11 (Sh. bil. 116.40) ni kwaajili ya nyongeza katika mchango wa Sweden katika Mpango wa Elimu kwa Matokeo(EP4R) ulioanza tangu mwaka 2015”, alifafanua.

Alisema fedha za kugharamia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu zitatumikakutimiza malengo mahsusi ya programu za Sekta ndogo za elimu ya msingi, elimujumuishi na watu wazima pamoja na elimu nje ya mfumo rasmi.

Alibainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo utachangia kwa kiasi kikubwakufikia malengo ya Mapango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano ambaopamoja na mambo mengine unalenga kuboresha Sekta ya Elimu kupitia Mafunzo yaKusoma, Kuandika na Kuhesabu (LANES), kuongeza udahili wa wanafunzi pamoja nakuboresha mazingira ya kusomea kwa kujenga madarasa.

Aliishukuru Serikali ya Sweden kwa kuratibu upatikanaji wa fedha hizi ambazozinafanya uwekezaji wa nchi hiyo hapa nchini kufikia zaidi ya shilingi trilioni1.25 zilizowekezwa kwenye miradi mbalimbali ikiwemo mapitio ya matumizi yafedha za Umma, maliasili na hifadhi ya jamii, elimu, nishati, utafiti, nakusisitiza kuwa uhusiano wan chi hizo mbili utaendelea kuimarika.

Aidha, Bw. James amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa jitihada zake kubwa za kusimamia miradimbalimbali ya maendeleo ikiwemo maboresho makubwa katika Sekta ya Elimu,ikiwemo utoaji elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

Naye Balozi wa Sweden Tanzania, Bw. Anders Sjoberg,  aliipongezaSerikali ya Tanzania kwa jitihada mbalimbali iliyochukua katika kuboresha elimuhususani katika awamu ya kwanza ya programu ya Mafunzo ya Kusoma, Kuandika naKuhesabu (LANES) pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2017 –2021.

Aliishauri Serikali ya Tanzania kuangalia kwa karibu suala la maendeleo yaelimu ya mtoto wa kike hasa kipindi cha kutoka elimu ya msingi kwenda Sekondaripamoja na kuboresha matokeo yao.

Alibainisha kuwa Sweden na washirika wengine wa maendeleo wapo tayarikushirikiana na Tanzania katika kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleoikiwemo elimu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DFID),Bi. Beth Arthy akizungumza kwa niaba ya washirika wengine wa maendeleo,ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua katika Sekta ya elimu ambayomatokeo yake yanaongezeka kila mwaka.

Alisema matokeo hayo yanatokana na mikakati mbalimbali iliyowekwa katikaSekta hiyo ikiwemo mpango wa elimu bila malipo ambao umeongeza idadi yawanafunzi na kuiwezesha Tanzania kujizolea umaarufu duniani.

Pamoja na maendelo hayo, Bi. Arthy aliishauri Serikali kuongeza idadi yawalimu mashuleni ili waweze kuhudumia wanafunzi kwa ufanisi na kuongeza ufauluzaidi.

“Tangu kuanzishwa kwa programu ya elimu bila malipo idadi ya wanafunzimashuleni imeongezeka kwa kasi tofauti na idadi ya walimu waliopo haliinayowafanya walimu kufanyakazi kubwa zaidi ya uwezo wao” aliongeza Bi. Arthy.

Akipokea msaada huo kwa shukrani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, alisema kuwa Wizara hiyo itahakikisha fedhahizo  zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha Elimu bora kwawote inapatikana Tanzania.

Msaada huoumechangiwa na washirika mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNICEF,UNESCO, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Australia, Canada, Denmark, Ufaransa,Korea, Uholanzi, Norway, Hispania, Uswiss, Marekani na Uingereza kupitia Mfukowa Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE)

Matangazo

  • TANGAZO LA ORODHA YA WADAIWA WA MALIPO YA VIWANJA AWAMU YA KWANZA KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA December 29, 2025
  • Tangazo na Orodha ya Walioitwa kwenye mafunzo ya Wasimamizi, Wasimamizi wasaidizi na Makarani Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba October 23, 2025
  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Tumetekeleza vizuri mkataba wa lishe 2024/2025

    January 23, 2026
  • Maaafisa utumishi acheni uonevu na kutumia lugha mbaya mnapotoa huduma- Prof Shemdoe

    January 20, 2026
  • Nitazunguka nchi nzima kuteta na watumishi wa afya ngazi ya msingi - Dkt. SEIF

    January 18, 2026
  • Afya ni kada ya huruna Dkt.Seif atoa wito kwa wanafunzi Mafinga

    January 18, 2026
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.

  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Toto Togel
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • KOI200
  • KOI200
  • Situs Toto
  • DORA77
  • Situs Toto
  • DORA77
  • DORA77
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Situs Toto Slot
  • Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • AXL777
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • AXL777
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot Gacor
  • situs toto
  • koi200
  • ufabet
  • ufabet
  • ufabet
  • ufabet
  • ufabet
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200
  • AXL777
  • AXL777
  • AXL777
  • AXL777
  • Situs Toto
  • situs toto
  • Toto Slot Gacor
  • AERO88 Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • AERO88
  • Situs Toto
  • situs toto
  • slot gacor
  • situs toto
  • yamitoto
  • kudetabet98
  • kudetabet98
  • yamitoto
  • dora77
  • koi200
  • aero88
  • yamitoto
  • axl777
  • dora77
  • dora77
  • aero88
  • aero88
  • dora77
  • dora77
  • slot gacor
  • axl777
  • axl777
  • yamitoto
  • axl777
  • axl777
  • axl777
  • axl777
  • axl777
  • axl777
  • yamitoto
  • axl777
  • aero88
  • dora77