Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Jafar Seif, amesema kwa sasa TAMISEMI imewekeza nguvu kwenye uboreshaji wa huduma kwa wateja katika vituo vyake vyote vya kutolea huduma za afya msingi ili kuhakikisha mpango wa huduma ya Bima ya Afya kwa wote unaendana na ubora wa huduma kwa wateja
Naibu Waziri, Dkt. Seif ameyasema hayo wakati wa kikao cha wataalum kutoka OWM-TAMISEMI, Wizara ya Afya na NHIF waliokutana Jijini Dar es Salaam leo Desemba 31, 2025, kupeana taarifa na kujengeana uelewa wa pamoja juu ya hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
Naibu Waziri Dkt. Seif amesema “TAMISEMI hatutalala, lazima tulifanikishe hili la kuboresha huduma za Afya kwa wateja wetu, tunataka lugha e staha na wahudumu wa Afya wawahudumie wagonjwa wetu kwa upendo ili tunapoanza matumizi ya bima ya afya kwa wote mapema 2026, basi Watanzania waione thamani ya bima hiyo kwa vitendo”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.