• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Rais Samia aweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato

Imewekwa tarehe: October 31st, 2022

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma huku akiwataka watanzania watakaopata fursa ya ajira katika  mradi huo kuacha vitendo vya wizi wa vifaa kwenye mradi huo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 31,2022 katika Kata ya Msalato Jijini Dodoma wakati wa hafla hiyo ambapo Mradi huo wa njia nne za Ndege utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 600 hadi kukamilika kwake.

Rais Samia amewasihi wananchi wa Dodoma na wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha kazi zinazoweza kufanya na watanzania wapewe kipaumbele.

“Ndugu zangu najua kuna tabia za baadhi ya wale mnaopewa kazi za muda(vibarua) wakipewa kusimamia ujenzi wanakuwa na vijitabia vya kudokoa dokoa mara Mfuko wa misumari,mara saruji hii sio sawa nataka mtakaopata nafasi msijihusishe na vitendo hivo,”amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia amesema kuwa ujenzi huo lengo ni kukuza ushindani unakuwepo wa kimataifa na pia ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwani ndege za kimataifa zitakuwa zikiendesha safari zake na pia soko la bidhaa litaongezeka.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame  Mnyaa Mbarawa  amesema Mradi huo utakuwa na fursa kwa Wakazi wa Dodoma na Mikoa mingine pamoja na kuiunganisha nchi na Mataifa mengine na kuahidi kusimamia ili ujenzi huo umalizike kwa wakati.

”Nia ya kujenga uwanja ilikuwepo tangu mwaka 1970 ambapo kiwango cha Ujenzi ni daraja E kwa mujibu wa viwango vya kimataifa na wataanza na ujezni wa barabara ya ndege kupaa kilomita 3.6 na utakuwa na uwezo wa kuwahudumia abiria Milioni 1.5 kwa mwaka.”amesema Prof.Mbarawa

Naye Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema Bunge litaendelea kumuunga mkono Rais Samia na kusema NDIYO kwenye bajeti ya Serikali kwa miradi mikubwa ya kimkakati na miradi mipya ambayo Serikali imepanga kutekeleza.

“Tumesikia hapa kuwa safari yako ya Ufaransa imewezesha kufanyika matengenezi makubwa ya jingo la pili la abiria katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, hivyo Bunge litaendelea kusema NDIYO kwa safari zako za nje. Hivyo ni kuahidi, Bunge litaendelea kusema NDIYO kwenye miradi ya maendeleo, tutakosoa panapobidi na kutoa ushauri.”

Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila, amesema kuwa eneo hilo lina ukubwa wa hekta 4500 na Sh.Bilioni 15.20 zimetumika kulipa fidia wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya mradi.

Mhandisi Mativila amesema kuwa mwaka 2015 serikali ilipata mkopo wa masharti nafuu kutoka AfDB kwa ajili ya marejeo ya upembuzi yakinifu na usanifu kwa kina ambapo mwaka 2017 serikali kupitia TAA iliingia mkataba na kampuni ya kihandisi ya nchini Tunisia kwa kampuni ya Tanzania kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 1.885 ambapo kazi hiyo ilikamilika mwaka 2019.

“Kiwanja hiki lengo kijengwe kiwe na uwezo wa kuhudumia abiria Milioni 32 kwa mwaka, kiwango ambacho kitafikiwa baada ya miaka 100,”

Naye , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema jumla ya wakazi wa Dodoma 3,368 wamelipwa fidia ya Sh bilioni 16.93 kupisha ujenzi huo ambapo wananchi 10 wanaodai fidia ya Sh milioni 80 wameshapelekwa maombi Hazina.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk Patricia Laverley,amesema kuwa ujenzi wa kiwanja hicho umefadhiliwa na benki yake kwa gharama ya dola za Marekani milioni 271 ambao utachukua miaka mitatu.

“Tunachotaka ni kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya Dodoma inavyotakiwa kuwa kwa kuimarisha usafiri anga kwa kuruhusu ndege za kimataifa kutua hapa nchini hatua ambayo itasaidia kuibadili Tanzania.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura, amesema mpaka Machi 2021 Tanzania ilikuwa na viwanja vya ndege 435 ambapo Serikali inamiliki viwanja 194 na viwanja vya sekta binafsi ni 241 ambapo viwango vya kimataifa vya ulinzi na usalama ni asilimia 69 kwa mwaka 2022 na lengo ni kufikia asilimia 75 katika kaguzi za mwaka 2023/24.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.