• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kata ya Hombolo Makulu yapata shule ya sekondari

Imewekwa tarehe: May 5th, 2022

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA

Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea na uboreshaji mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Kata ya Hombolo Makulu baada ya kupokea shilingi milioni 470 kupitia mradi wa SEQUIP.

Akizungumza na mwandishi wetu, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari wa Jiji la Dodoma, Mwalimu Upendo Rweyemamu alisema kuwa ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa SEQUIP unaotekelezwa kwenye eneo la Elimu ya Sekondari kuanzia kidato cha 1 – 6 kwa muda wa miaka mitano (5) kuanzia mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 nchi nzima na utekelezaji wake umeelekezwa kwenye maeneo ya vipaumbele vya Serikali yanayogusa moja kwa moja elimu ya sekondari. Shule mpya za sekondari 1,000 zinajengwa nchini katika kata ambazo hazina shule za sekondari na maeneo ambayo yana wanafunzi wengi ukilinganisha na miundombinu iliyopo.

Amesema kuwa mradi huo unahusisha pia ujenzi wa shule mpya za sekondari za wasichana za mikoa 26 ambapo kila mkoa inajengwa shule moja.

“Hadi sasa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepokea awamu ya kwanza kiasi cha shilingi 470,000,000 (milioni mia nne na sabini) za ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma Makulu. Ujenzi huu unahusisha vyumba nane vya madarasa, maabara tatu za sayansi (kemia, biolojia na fizikia), jengo la utawala, maktaba, chumba cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Matundu 20 ya vyoo vya wanafunzi (wasichana matundu 10 na wavulana matundu 10), tanki la maji la lita 10,000, ujenzi wa nguzo ya kuwekea tanki, Ujenzi wa miundombinu ya kunawa mikono na miundombinu ya kuvuna au kuunganisha maji”, alisema Mwalimu Rweyemamu.

Mradi huo umelenga kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ya sekondari, kuweka mazingira salama ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu bora ya sekondari. Shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiopungua 400 kuanzia kidato cha Kwanza hadi cha Nne, aliongeza Mwalimu Rweyemamu.

Naye Issa Kambi, Afisa Elimu maalum katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, akiwa katika eneo la mradi alisema “ujenzi katika mradi huu ulianza rasmi mwezi Januari mwaka huu, na kama unavyoona ujenzi upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji wa majengo yote”.

Kiasi cha shilingi 408,000,000 (milioni mia nne na nane) kimeshatumika na awamu hii ya kwanza ya ujenzi inatarajiwa kukamilika tarehe 30 Mei, 2022 na awamu ya pili ya mradi huu itahusisha ujenzi wa nyumba za walimu na ununuzi wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mafundi wakiendelea na ukamilishaji wa jengo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Moja ya majengo ya maabara ya sayansi likiwa katika hatua ya ukamilishaji.

Madarasa yakiwa katika hatua ya umaliziaji.

Matangazo

  • Tangazo la nafasi za ajira za Jeshi la Magereza kwa mwaka 2022 June 02, 2022
  • Tangazo la nafasi za kazi Jiji la Dodoma May 27, 2022
  • Tangazo kuhusu zoezi la Anuani za Makazi na Postikodi April 30, 2022
  • Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2022 April 28, 2022
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Julai 7 Siku ya Kiswahili Duniani, Quatar yaalikwa

    June 23, 2022
  • Sumbawanga wafurahia elimu kutoka Dodoma Jiji

    June 22, 2022
  • Wete, Dodoma Jiji kukuza ushirikiano

    June 22, 2022
  • Mavunde aipongeza Mbeya kutenga mashamba makubwa ya kilimo cha soya

    June 20, 2022
  • Angalia zote

Video

Chang'ombe wampongeza Diwani wao, utatuzi kero za elimu, afya
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    3 CDA Street

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.