• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Halmashauri za Dodoma igeni Jiji la Dodoma - RAS Mganga

Imewekwa tarehe: January 16th, 2022

HALMASHAURI za Mkoa wa Dodoma zimetakiwa kuiga mfano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutenga shilingi Bilioni 7.5 katika mapato yake ya ndani kujenga jengo la kisasa la Machinga ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri.

Ushauri huo ulitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatuma Mganga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi jengo la kisasa Machinga katika eneo la Bahi road jijini Dodoma iliyofanyika siku ya Alhamisi tarehe 13 Januari, 2022..

Dkt. Mganga alisema “nichukue fursa hii kusema neno moja, mradi huu ni mkubwa wa shilingi bilioni saba pointi. Hiyo bilioni saba haijatoka serikali kuu, lazima tulifahamu hili. Hii bilioni saba ni mapato ya ndani ya Jiji la Dodoma. Tunaposema kutumia asilimia 40 kuleta maendeleo hii ndilo tunalolieleza. Kwamba tunasubiri kwamba kila mradi mkubwa fedha zitoke serikali kuu, lakini katika hili iwe mfano, kama hii Machinga complex inajengwa kwa mapato ya ndani ya Jiji hii ndiyo ile kauli ya viongozi wetu wanavyosema fedha tunazokusanya kwenye mapato ya ndani ya halmashauri zitumike kuleta maendeleo katika halmashauri. Katika hili, Jiji wanapaswa kupongezwa sana. Hili ni funzo, halmashauri zetu nyingine za Mkoa wa Dodoma ziige mfano huu. Tuwe na miradi ya asilimia 40 yenye tija ambayo inaonekana kabisa hizo fedha thamani yake inaonekana na inakwenda kutatua changamoto za wananchi moja kwa moja. Katika hili Jiji niwapongeze sana”.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa eneo hilo linalojengwa lina uwezo wa kuweka Machinga 3,000 na kuongeza kuwa eneo hilo linauwezo wa kuongeza Machinga hadi kufikia 5,000. “Kama tulivyokubaliana kwenye kikao cha ndani tunaendelea kusajili Machinga wote kwa njia ya kieletroniki ili wale tulioanza nao 3,000 wa kwanza wawe wa mwanzo kuingia katika mradi huu” Sisi kama Jiji ambacho tunaweza kukuhakikishia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa fedha tunayo tumetenga kwenye bajeti. Tutamsimamia Mkandarasi ili akamilishe kama tulivyokubaliana kufikia tarehe 17 Machi, 2022 atukabidhi mradi ili uanze kutumika” alisema Mkurugenzi Mafuru.

Aidha, alimhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa halmashauri itasimamia ili anayefanya kazi eneo hilo awe ni mtu anayestahili. “Hii mambo ya kujipachika ndiyo maana tunakwenda kwenye mfumo wa kietroniki. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa mpaka sasa toka tuanze hatujapata changamoto yoyote tupo kwenye muda. Mkandarasi tumeshamlipa shilingi Milioni 841 kwa ajili ya kuendelea na mradi huu. Tunaimani mradi huu ukikamilika Dodoma itakuwa safi” alisema Mkurugenzi Mafuru.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alifanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la kisasa la Machinga akiambatana na Katibu Tawala Mkoa, Kamati ya Usalama ya Mkoa, viongozi wa Chama cha Mapinduzi na maafisa waandamizi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Matangazo

  • Tangazo kuhusu zoezi la Anuani za Makazi na Postikodi April 30, 2022
  • Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2022 April 28, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye USAILI WA MAHOJIANO kwa nafasi za Kazi ya Kukusanya Taarifa za Anwani za Makazi na Postikodi March 04, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa nafasi za Kazi ya Kukusanya Taarifa za Anwani za Makazi na Postikodi February 28, 2022
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Serikali kujenga 'Sports and Arts Arena' Dodoma na Dar

    May 24, 2022
  • Rais Samia ziarani nchini Ghana

    May 23, 2022
  • Wakulima Milioni 1 kunufaika na programu ya mkopo wa pembejeo na soko la mazao

    May 20, 2022
  • Tanzania yafikia lengo uwekaji wa Anwani za Makazi - Waziri Nape

    May 20, 2022
  • Angalia zote

Video

DC Shekimweri awakumbusha wakazi Mtumba kutumia vema fedha za fidia
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    3 CDA Street

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.