Na Angela Msimbira, Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha hakuna mtoto anayezuiwa kuanza au kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sare, wakati shule zote nchini zikitarajiwa kufunguliwa rasmi Januari 13, 2026
Prof. Shemdoe amesema kuwa agizo hilo linapaswa kusimamiwa kikamilifu katika maeneo yote ya nchi ili kuhakikisha kila mtoto anapokelewa shuleni bila masharti yanayokiuka miongozo na sera za elimu.
Amesisitiza kuwa mara mtoto anapopokelewa shuleni, masuala mengine ikiwemo sare, yataendelea kushughulikiwa akiwa tayari anaendelea na masomo, hatua itakayosaidia kuondoa vikwazo vinavyowafanya baadhi ya watoto kukosa haki yao ya msingi ya elimu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.