MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma anawatangazia wananchi wote wanaodaiwa malipo ya viwanja katika maeneo ya Mtumba Zone II, Mtumba Zone III na Kikombo kuwa awamu ya kwanza ya orodha yao imetolewa katika vyombo vya habari na wamepewa siku 21 kuweza kukamilisha malipo hayo kunzia tarehe 30 Desemba, 2025.
Aidha, iwapo mwananchi, taasisi au kampuni amekamilisha malipo na jina lake lipo katika orodha hii anashauriwa kufika halmashauri akiwa na nyaraka zake halisi (original) kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.
Baada ya siku 21 kumalizika, halmashauri itavirudisha sokoni viwanja vyote ambavyo malipo yake hayajakamilika.
Orodha hii inapatikana katika Gazeti la Mwananchi la tarehe 30 Desemba, 2025, Tovuti www.dodomacc.go.tz na mitandao ya kijamii ya halmashauri Instagram @dodomacc_tz, Facebook Dodoma Council.
Kuona orodha ya wadaiwa bofya hapa:-
Kwa maelezo zaidi fika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ofisi za iliyokuwa Manispaa ya zamani, Duka la kuuzia viwanja, Namba 03, au piga Simu Namba 0754 551 694 au barua pepe: cd@dodomacc.go.tz
Tangazo hili limetolewa na: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.